YANGA KUPIMANA UBAVU NA SINGIDA BLACK STAR

Klabu ya Singida Black Stars ya mjini Singida, Machi 24 inatarajiwa kuzindua uwanja wake mpya ambao huenda ukaanza kutumika katika mechi za kuhitimisha msimu huu.

Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 5,000 hadi 7,000 utazinduliwa kwa mechi ya kirafiki kati ya Singida Black Stars dhidi ya Yanga

Wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA, mechi hiyo pia itatumika kama sehemu ya maandaliuzi ya timu zote kuelekea mechi za kuhitimisha msimu huu wa 2024/2025.

Yanga na Singida Black Stars tayari zimemalizana kwenye ligi huku Yanga ikishinda mechi zote.

Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza na kushinda bao 2 - 0 katika mechi ya mkondo wa pili.

Post a Comment

0 Comments