Jana shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) liliweka hadharani ratiba ya mechi za hatua ya 16 bora kombe la shirikisho la CRDB ambapo Yanga itashuka dimbani Machi 29 kumenyana na Songea United.
Mchezo huo wa kuwania tiketi ya kutinga robo fainali utapigwa uwanja wa KMC Complex na baada ya mchezo huo wananchi watakuwa na siku mbili za mapumziko kabla ya kuikabili Tabora United katika mchezo wa ligi kuu NBC ambao umepangwa kufanyika APril 1, 2025.
Bado haijafahamika mchezo dhidi ya Tabora United utapigwa katika uwanja upi kwani dimba la Ali Hassan ambako Tabora walicheza mechi yao iliyopita vimefungiwa na bodi ya ligi
0 Comments