Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry
Na Isaac Masengwa
*******************
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Daktari Daniel Henry Mono amepewa mapokezi makubwa na waumini wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayofanya kazi katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Mapokezi hayo makubwa yakiongozwa na Askofu wa dayosisi hiyo Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu, yamekuwa mapokezi ya kwanza tangu ateuliwe kuwa askofu wa dayosisi ya Mwanga na yamefanyika leo Machi 15, 2025.
Akizungumza katika sala fupi ya mapokezi hayo iliyofanyika katika usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga, Askofu mteule Daktari Daniel Henry Mono amesema kuwa hakutegemea kukutana na mapokezi makubwa kama haya.
"Kwa kweli leo nimetekewa kwa sababu ukweli kabisa sikujua kama kuna jambo la namna hii. Nimekutana na jambo ambalo sikulitegemea kabisa, nimeona magari, watu na tarumbeta ambapo nilijikuta nikitekewa"
"Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa yote aliyotenda, ninamshukuru kwa jinsi alivyonipitisha katika utumishi wake na mpaka sasa ameniita tena kutumika katika nafasi hii kubwa."
"Pia nikushukuru sana baba Askofu Yohana Ernest Nzelu, umekuwa rafiki yangu kwa muda mrefu, nimeishi na wewe kama rafiki na kama ndugu. Hata ulipofika wakati wa kufanya kazi na wewe nimefurahi sana kufanya kazi na mimi. Pia nikushukuru hata kwa jinsi umenishauri katika kuliendea jambo hili."
"Lakini pia nikushukuru sana baba Askofu mstaafu Makala, umekuwa mwalimu wetu mwema katika utumishi huu. Umenipa malezi mazuri ya kiutumishi, umetuntengeneza hadi kuwa hivi nilivyo. Kupata nafasi kama hii wewe umekuwa sehemu ya kufikia hatua hii."
Naye Askofu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Daktari Yohana Ernest Nzelu, amemshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii ya utumishi aliyoipata askofu mteule Daktari Mono.
"Ni haki yetu kama dayosisi kumshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi hii aliyoipata
"Nimshukuru sana Baba Askofu mstaafu Daktari Emmanuel Makala kwa kuwa yeye ndio amekuwa lango la wengine kupata nafasi kama hizi. Katika utumishi wako umekuwa chanzo cha sisi wengine kupata nafasi hizi."
"Nimepokea barua kutoka dayosisi ya Mwanga wakiniomba Daktari Mono uende ukatumike katika dayosisi ya Mwanga".
"Nami nimewajibu majibu ya awali kuwa Daktari Mono atakuja kutumika katika dayosisi ya Mwanga tukiwa tunasubiri maamuzi ya mwajiri wake"
Naye kwa upande wake askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo Askofu Makala amempongeza Askofu mteule Daniel Mono na kumtaka kuwa kiongozi atakayeandaa viongozi wajao.
"Ukipewa nafasi ya kuongoza andaa wengine ili kanisa liweze kusonga mbele. Baba askofu mteule hongera sana, wewe nenda kafanye kazi ya Mungu kwa kadri Mungu atakavyokutumia."
Daktari Daniel Henry Mono ni msaidizi wa Askofu wa dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria. Na alichaguliwa na mkutano mkuu wa dayosisi ya Mwanga iliyopo mkoani Kilimanjaro kuwa askofu wa pili wa dayosisi hiyo yeye akiwa katika majukumu yake Nchini Burundi.
Hii inakuja baada ya aliyekuwa Askofu wa kwanza wa dayosisi hiyo Chediel Sendoro kufariki dunia mwaka jana Septemba 9, 2024 kwa ajali ya gari

Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akitoa neno la shukrani kwa waumini wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakati wa mapokezi

Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akiongoza mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Askofu Daktari Yohana Ernest Nzelu akiongoza mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi akitoa maelekezo wakati wa mapokezi yaAskofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akiwasili usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakati wa mapokezi hayo

Mama Askofu mteule Heavenlight Daniel Mono akifuatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi hayo
Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Emmanuel Joseph Makala akizungumza machache wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono
Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Emmanuel Joseph Makala akizungumza machache wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono.

Askofu mstaafu Daktari Emmanuel Makala (katikati), Mama Askofu mstaafu Mdiakonia Lilian Makala (kushoto) na Chaplain wa Kanisa Kuu Mchungaji Zinyangwa Silas Mkiramweni wakifuatili kwa makini tukio la kumpokea Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Henry Mono

Akofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu (kulia) na Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi (kushoto) wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Henry Mono

Askofu
mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono (kushoto) akiwa na
mwenyeji wake Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu wakati wa mapokezi hayo
Askofu
Daktari Yohana Ernest Nzelu akifuatilia kwa makini kinachoendelea
wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa Dayosisi ya Mwanga Mchungaji
Daktari Daniel Henry Mono

Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Mono akifauatilia kwa makini kinachoendelea wakati wa mapokezi yake mkoani Shinyanga
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi akifuatilia kwa umakini kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga

Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono (kulia), Askofu
wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Mchungaji Daktari Yohana Ernest Nzelu (katikati) Mama Askofu Lilian
Yohana Ernest Nzelu (katikati) na Mama Askofu mteule Heavenlight Daniel
Mono (kulia) wakiwa wanafuatilia kinachoendelea wakati wa mapokezi hayo

Wachungaji
wa KKKT Dayosisi Kusini mashariki wakifuatilia kwa makini
kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya
Mwanga

Wachungaji
wa KKKT Dayosisi Kusini mashariki wakifuatilia kwa makini
kinachoendelea wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya
Mwanga

Kwaya
ya Muungano ya watumishi wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki Ofisi kuu za
Dayosisi pamoja na watumishi wa Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu
Shinyanga wakiimba wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi
ya Mwanga

Waumini
na Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
wakimlaki kwa shangwe na kumpongeza Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya
Mwanga wakati wa mapokezi

Waumini
na Wachungaji wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
wakimlaki kwa shangwe na kumpongeza Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya
Mwanga wakati wa mapokezi
Msafara wa magari wakati wa mapokezi ya Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mchungaji Daktari Daniel Mono

Tags:
habari