
Ajali mbaya imetokea eneo la Gongolamboto mwisho, kwenye kilima cha kuingia Pugu Sekondari, na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Chanika (OCD), Awadh Mohamed Chiko.
Kwa mujibu wa mashuhuda, daladala la aina ya Eicher lilitanua na kufuata upande wa gari la OCD Awadh, ambaye alikuwa akiendesha Toyota Prado, na kusababisha ajali hiyo mbaya.
Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali na hatua zinazochukuliwa na vyombo vya usalama zitaendelea kufuatiliwa.