
MCHUNGAJI kutoka Togo, Apostle Elijah Ayeh Courage, amezua gumzo mtandaoni baada ya video zake zikimuonyesha akihubiri akiwa amevaa viatu virefu vya kisigino (high heelss) kusambaa kwa kasi.
Mchungaji huyo kutoka mji mkuu wa Togo, Lomé, amesema kuvaa viatu hivyo si suala la mtindo wa mavazi, bali ni maagizo aliyoyapokea kutoka kwa Roho Mtakatifu miaka kadhaa iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Apostle Courage havai viatu vya high heels kanisani pekee, bali huvitumia muda wote, hata akiwa nyumbani.
Akizungumza kuhusu sababu ya kuchagua mtindo huo wa kipekee, alisema:"Roho Mtakatifu alinielekeza nivivae ili niweze kufanikisha kazi ya kuhubiri kwa ufanisi zaidi."
Hata hivyo, mtindo wake umeibua maoni mseto, huku baadhi wakimpongeza kwa uthubutu wake, wakati wengine wakimkosoa kwa kile wanachokiita kuvunja mila na desturi za kidini.
Katika moja ya mahubiri yake, Apostle Courage alijibu wakosoaji wake kwa kusema: "Wengine wanaona mavazi yangu kuwa ni machukizo, lakini dhambi ya kweli imo kwenye mawazo na matendo maovu ya wanadamu, si kile mtu anachovaa."
Je, ni kweli Roho Mtakatifu alimwelekeza kuvaa viatu hivyo, au kuna jambo jingine nyuma ya pazia?

0 Comments