WASIRA AMTAKA MO DEWJI KURUDISHA MASHAMBA MARA MOJA

 


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Bw. Stephen Wasira amemtaka mmiliki wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Bw. Mohamed Dewji kurudisha mashamba ya chai anayomiliki Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya kwa Serikali kama ameshindwa kuyaendesha na kubaki vichaka vya wanyama waharibifu kwa binadamu huku wananchi wakiendelea kutaabika kwa kukosa maeneo ya kufanya shughuli za kiuchumi.

Bw. Wasira ametoa maagizo hayo baada ya wananchi waliofika kwenye mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero uliofanyika katika Kituo cha Mabasi Rungwe.

Chanzo : ITV

Post a Comment

0 Comments