TABORA UNITED WAPANIA KUICHAKAZA KMC
NYUKI wa Tabora, Tabora United wapo ndani ya jiji la Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi inayofuata ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wakusanya mapato wa Kinondoni, KMC.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 jioni ambapo wababe hao wawili watakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu.
Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita kwa KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji ilikuwa Novemba 24 2024.
Tabora United yene Ofeen Chikola, Heritier Makambo, Haron Mandada wao walikomba pointi moja kwa ubao kusoma Tabora United 2-2 Singida Blacks Stars baada ya mchezo huo aliyekuwa Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Patrick Aussems alikutana na Thank You.
Christina Mwagala, Ofisa Habari wa Tabora United amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo muhimu na ambacho wanahitaji ni pointi tatu.
“Tunatambua utakuwa mchezo mgumu, wachezaji wapo tayari kikubwa ni kuona kwamba tunavuna pointi tatu mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu muhimu.”
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: