Polisi wamnasa mtu mmoja na misokoto 447 ya bangi

JESHI la Polisi Manyara linamshikilia mtu mmoja kwa kusafirisha misokoto 447 ya bangi, ambayo alihifadhi kwenye ndoo na kuweka juu ya unga wa sembe ili kupoteza ushahidi wa kufahamika kwa bangi hiyo.


Kamanda wa Polisi Francis Massawe, jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, wakati maaskari walipokua doria ndipo walipomtia nguvuni mtuhumiwa.

“Mtu huyo alikamatwa Desemba 27, wakati askari walipokuwa kwenye misako na operesheni za kawaida huko katika kata ya Bonga akiwa ndani ya gari namba T.912 BFA lililokuwa likitokea Arusha kuelekea Kondoa,’’ alisema Massawe.

Kamanda Massawe hakumtaja majina kwa sababu za kiuchunguzi ila alidai anaumri wa miaka (35) ni mwanaume kutoka kijiji cha Mwongozo, kilichopo wilaya ya Kondoa vijijini.

Massawe alisema basi alilokuwa amepanda ni aina ya Nissan, ila halikuweza kujulikana la kampuni gani kwa kuwa lilikuwa halijaandikwa jina lolote.

Source: Nipashe

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.