HABARI MPYA KUTOKA YANGA SAA CHACHE KABLA YA MECHI DHIDI YA AZAM

Baada ya mapumziko ya kalenda ya CHAN, Ligi kuu NBC inarejea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wataumana na Azam FC katika uwanja utakaopigwa katika uwanja qa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
Ni dabi ya jijini Dar es Salaam, ukitoa mchezo wa watani wa jadi ,mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam FC unashika nafasi ya pili kwa ukubwa
Nje ya uwanja mashabiki wanaamini Azam FC na Simba ni kama kaka na dada hivyo ushindi dhidi ya Azam utapeleka maumivu msimbazi na ni hivyo hivyo kinyume chake ushindi wa Azam utapeleka furaha Msimbazi
Mara nyingi timu hizi zinapokutana mchezo huwa sio mwepesi, dakika 90 ndizo zinazoamua matokeo
Yanga imewek rekodi ya kucheza mechi 39 pasipo kupoteza lakini timu ya nwisho kuifunga Yanga ilikuwa timu ya Azam FC, April 25, 2021katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ulikuwa mchezo wa kwanza na pekee kwa kocha Nasreddine Nabi kupoteza tangu alipojiunga na Yanga mwanzoni mwa April 2021
Nabi amesema licha ya kikosi chake kushinda mechi zote mbili msimu uliopita hawapaswi kubweteka kwani watahitaji kupambana ili kuweza kushinda siku ya leo
Wakati Yanga kikosi chao kina mabadiliko kidogo, Azam wamefanya usajili mkubwa wakisajili nyota wengi mahari
Hata hivyo Azam FC walianza msimu kwa kusuasua wakishinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja katika dimba lao la Azam Complex matokeo yaliyopelekea kufanya mabadiliko ya benchi lao la ufundi
Utakuwa mchezo wake wa kwanza Yanga kucheza katika uwanja wake wa nyumbani kwenye ligi msimu huu, michezo miwili ya kwanza walicheza mkoani Arusha dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union na kufanikiwa kushinda yote
Mchezo utapigwa kuanzia saa moja usiku
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: