TANESCO NA EWURA WAWAJENGEA UWEZO WATAALAMU WA KUFUNGA MIFUMO YA UMEME SHINYANGA

Afisa Uhusiano na huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Emma Nyaki akizungumza wakati wa mafunzo hayo 
Mhandisi wa Umeme John Francis Kitonga kutoka EWURA Kanda ya Magharibi akitoa mada wakati wa mafunzo hayo
 Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Kisika Eliya Kisika, akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwenye mafunzo kwa Wataalam wa Kufunga Mifumo ya Umeme Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kusaidia kuboresha ufanyaji kazi wao
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wataalam wa Kufunga Mifumo ya Umeme Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kusaidia kuboresha ufanyaji kazi wao

Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, wametoa mafunzo kwa wataalamu wa kufunga mifumo ya umeme 'Wakandarasi wa umeme' mkoani Shinyanga. 

Mafunzo hayo  yaliyolenga kuwajengea uwezo wataalam hao ili kuboresha ufanyaji kazi wao, na kuhakikisha huduma wanazozitoa zinakuwa bora, salama na zinazofanyika kwa viwango vinavyokubalika yamefanyika leo, Jumanne Februari 4, 2025, katika ukumbi wa Mikutano wa Planet Hotel, Mjini Kahama.

Watalaam hao wamejengewa uelewa wataalam hao kuhusu majukumu ya EWURA, kanuni za umeme za mwaka 2022, makundi na madaraja ya leseni, pamoja na namna ya kufanya maombi ya leseni kupitia mfumo mpya wa maombi (LOIS-Mpya) na pia wamejifunza namna ya kujaza fomu za kukamilisha shughuli za ufungaji mifumo ya umeme.

Akifungua semina hiyo, Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher, amesema kuwa semina hiyo ni fursa kwa wataalam wa umeme kuelewa kanuni, miongozo na mifumo ya udhibiti ya sekta ya umeme. 

Amesema kuwa elimu hii itawasaidia kuepuka kuvunja sheria, na hivyo kuepuka adhabu za kutozwa faini au kufutiwa leseni.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher.

“EWURA inatoa fursa ya kuzungumza na wataalamu mara kwa mara, ili kuhakikisha wanapata uelewa wa kina kuhusu mabadiliko ya kisheria na kiudhibiti, na namna bora ya kuwahudumia wateja wao,” amesema Mhandisi Christopher.

 “Mafundi wote wa umeme wanapaswa kujaza fomu ya kukamilisha kazi baada ya kumaliza ufungaji au matengenezo ya mifumo ya umeme. Hii ni muhimu ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ubora na viwango vya juu”,ameongeza.

Mhandisi Christopher amesisitiza kuwa EWURA inahakikisha kuwa kazi za ufungaji mifumo ya umeme zinatekelezwa na wataalam walio na leseni pekee. 
Ameongeza kuwa, taasisi kama TANESCO, Halmashauri, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wanapaswa kuhakikisha kuwa kazi za ufungaji mifumo ya umeme zinazotolewa kwa mafundi ni kwa wale walio na leseni sahihi kutoka EWURA.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa mifumo ya umeme inafungwa na wataalam wenye weledi na ujuzi katika fani hii, ili mteja apate huduma bora, salama na inayokidhi viwango vya afya, mali na mazingira,” amesema.

Aidha, Mhandisi Christopher amefafanua kuwa EWURA inashirikiana na vyuo kama vile VETA ili kuwajengea uwezo wanafunzi na kuwahimiza kuomba leseni pindi wanapohitimu masomo yao.

Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Kisika Eliya Kisika, akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga amekumbusha wataalam wa umeme wasiokuwa na leseni watafute leseni lakini pia kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na kuepuka tamaa.
Mhandisi Kisika Eliya Kisika.

Aidha amewataka wataalam wa umeme kupendana na kufanya kazi kushirikiana na kama wana changamoto wasisite kuwasiliana na TANESCO.

 Amesema TANESCO itahakikisha wateja wake wanahudumiwa kwa wakati, na kuwa wataalam hao wanapaswa kuwaelimisha wateja kuhusu umuhimu wa kukagua mifumo ya umeme.

Wataalam wa mifumo ya umeme wameishukuru TANESCO na EWURA kwa kuwapatia mafunzo haya ambayo yatawasaidia kufanya kazi kwa weledi na kuepuka migogoro, wakiaahidi kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa ili kuepuka adhabu na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja wao.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wataalam wa Kufunga Mifumo ya Umeme Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kusaidia kuboresha ufanyaji kazi wao ili kuhakikisha kuwa huduma wanazotoa zinakuwa bora, salama na zinazofanyika katika viwango vinavyokubalika yaliyofanyika leo Jumanne Februari 4,2025 Mjini Kahama - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wataalam wa Kufunga Mifumo ya Umeme Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kusaidia kuboresha ufanyaji kazi wao
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wataalam wa Kufunga Mifumo ya Umeme Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kusaidia kuboresha ufanyaji kazi wao
 Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Kisika Eliya Kisika, akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwenye mafunzo kwa Wataalam wa Kufunga Mifumo ya Umeme Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kusaidia kuboresha ufanyaji kazi wao
 Katibu wa Wakandarasi wa Umeme Wilaya ya Kahama, Six Mbuki akizungumza kwenye mafunzo kwa Wataalam wa Kufunga Mifumo ya Umeme Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kusaidia kuboresha ufanyaji kazi wao
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Kishapu, Neema Robert Ngh’ome akizungumza kwenye mafunzo hayo
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Kishapu, Neema Robert Ngh’ome akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mhandisi wa Umeme John Francis Kitonga kutoka EWURA Kanda ya Magharibi akitoa mada wakati wa mafunzo hayo
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Shinyanga Robert Msemo akizungumza kwenye mafunzo hayo
Meneja wa TANECO Wilaya ya Kishapu Mhandisi Hussein Mbulu akizungumza kwenye mafunzo hayo
Meneja wa TANECO Halmashauri ya Ushetu, Mhandisi George Madaha akizungumza kwenye mafunzo hayo
Meneja wa TANECO Halmashauri ya Msalala, Mhandisi Kitila Bryson akizungumza kwenye mafunzo hayo
Wataalamu wa kufunga mifumo ya umeme  wakiwa ukumbini.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.