WANANDOA WALIOFANYA NGONO KATIKATI YA BARABARA MCHANA KWEUPE WATUPWA JELA MIEZI 30

Wanandoa waliohukumiwa miezi 30 jela

Wanandoa nchini Uganda wamehukumiwa kifungo cha miezi 30 jela baada ya kunaswa kwenye video wakishiriki tendo la ndoa katikati ya barabara inayotumiwa na watu wengi mchana kweupe.

Video ya wapenzi hao wawili ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadaye walikamatwa na jeshi la polisi nchini humo na kufikishwa mahakamani.

Wanandoa hao Paskari Hafashimana (29), na mpenzi wake Colodine Mukamulenzi Muhawenimana (24), walionekana kwenye video hiyo wakifanya tendo hilo kwenye barabara ya Kisoro-Bunagana.

Wakisomewa mashtaka yao wanandoa hao walikubali kutenda kosa hilo na waliomba wapunguziwe adhabu, lakini Hakimu aliamuru wafungwe jela kwa muda wa miezi 30.

Chanzo: Tuko swahili

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.