NCHI 10 TAJIRI ZAIDI BARANI AFRIKA

Bara la Afrika linatajwa kuwa maskini zaidi duniani, huku umaskini wa bara hilo ukichangiwa na hali ya uchumi kuyumba, ukosefu wa usalama, ufisadi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na vitendo vya kigaidi katika bara hilo.
Shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia, katika ripoti ya pamoja iliyochapishwa mwishoni mwa 2021, zimetangaza nchi 10 tajiri zaidi barani Afrika.
1. Misri

Misri imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na ukuaji wa juu wa uchumi kulingana na ripoti hiyo.
Mapato ya kila mwaka ya Misri ni $1.38 trilioni.
Misri ina jumla ya watu milioni 102, na nchi hiyo inategemea kilimo, uchimbaji madini na utalii.
2. Nigeria

Nigeria, ambayo ni ya pili kwa utajiri barani Afrika, ina pato la taifa la dola trilioni 1.14. Nigeria ina jumla ya watu milioni 206.1, ikiifanya kuwa nchi yenye watu wengi zaidi Afrika Uchumi wa Nigeria unategemea mafuta na kilimo.
3. Afrika Kusini

Afrika Kusini, ambayo ni nchi tajiri zaidi barani Afrika, inaorodheshwa ya tatu ikiwa na pato la taifa (GDP), inayofikia dola bilioni 861.93 kwa mwaka.
Nchi hiyo ina watu 59,899,576, uchumi wake unategemea madini , hususan dhahabu na mali asili nyingine.
4. Algeria

Algeria ni nchi ya tatu tajiri zaidi barani Afrika, na pato la taifa (GDP) ni dola bilioni 532.57.
Nchi hiyo ina watu 44,911,520 na uchumi wake unategemea mafuta na gesi asilia inayouzwa nje ya nchi.
6. Ethiopia

Ethiopia, ambayo iko Afrika Mashariki na kushika nafasi ya sita kati ya nchi tajiri zaidi barani Afrika, ina Pato la Taifa la $298.57 bilioni kwa mwaka.
Ethiopia ina wakazi milioni 115 na uchumi wake unategemea Kilimo .
7. Kenya

Kenya, ambayo inapatikana eneo la Afrika Mashariki na imeorodheshwa ya saba miongoni mwa kumi tajiri zaidi barani Afrika, ina Pato la Taifa la kila mwaka la $269.29 bilioni.
Kenya ina watu 54,039,625, na uchumi wake unategemea kilimo, utalii na biashara.

8. Angola
Angola, ambayo iko eneo la kati mwa Afrika, inaorodheshwa ya nane miongoni mwa nchi kumi tajiri zaidi barani Afrika. Ina Pato la Taifa la kila mwaka la bilioni 217.97 za Kimarekani.
Angola ina jumla ya watu 35,601,398, na uchumi wake unategemea mafuta na madini.
9. Ghana

Ghana, ambayo ipo magharibi mwa Afrika inaorodheshwa ya tisa miongoni mwa nchi 10 tajiri zaidi katika bara la Afrika ina jumla ya pato la dola bilioni 193.63 kwa mwaka.
Ghana ina watu 33,483,283, na uchumi wake unategema uzalishaji wa viwanda kama vili teknolojia na uchukuzi.
10. Sudan

Hatimaye, Sudan, ambayo ipo katika eneo la Afrika Mashariki, inaorodheshwa ya 10 miongoni mwa nchi tajiri barani Afrika, ikiwa na pato la taifa la dola bilioni 189.87 za Kimarekani kwa mwaka.
Sudan ina watu 46,888,316, na uchumi wake unategemea mafuta na kilimo.
Ripoti hiyo ilisema kuwa bara la Afrika lina mali asili nyingi, lakini nchi katika bara hilo zinatumia mali hizo kuzua vita, ufisadi na misukosuko ya kisiasa ambayo imechangia masuala haya.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: