KUUMIA KWA YACOUB KUMELETA TAFRANI KWENYE KIKOSI CHA YANGA...NABI AFANYA MAAMUZI MAGUMU
KOCHA wa Yanga amefunguka kuwa, kambi yao ya Zanzibar imekuwa na mafanikio na sasa amepata mifumo mipya itakayobdili sura ya kikosi chake hasa baada ya Yacouba Songne kuumia na kuendelea na matibabu nchini Tunisia.
Yanga itarudi katika Ligi Kuu baada ya kusimama kwa wiki mbili kupisha mechi za kimataifa kwa timu za taifa, Jumamosi ikiifuata Namungo kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi bila ya kuwa na mshambuliaji huyo.
Akizungumza na hivi karibuni, Kocha Nabi alisema kukosekana kwa Yacouba inamlazimisha kubadili mbinu zake na hata sura ya kikosi chake itabadilika kidogo.
Nabi aliyeiwezesha Yanga kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa alama 15 kupitia mechi tano, alisema Yacouba alikuwa akifanya kazi kubwa akitokea pembeni kushoto alilokuwa anatengeneza nguvu kubwa kati ya safu ya ushambuliaji na ile ya kiungo na sasa anatakiwa kupiga hesabu upya.
“Hatukuwa tu tunacheza mechi za kirafiki na kufanya mazoezi Zanzibar, bali kulikuwa na kazi pia ya kutafuta mifumo mipya ambayo tutaitumia kuanzia sasa hasa baada ya kuumia kwa Yacouba,” alisema Nabi na kuongeza;
“Kumkosa Yacouba ni pengo tunamuombea apone haraka, lakini maisha lazima yaendelee tunatakiwa kuwa na akili mpya ya jinsi tutakavyocheza sasa na nani ataingia eneo hilo au kwingine.”
Nabi aliongeza anasubiri kurejea salama kwa wachezaji wake waliopo timu za taifa, na kwamba kila aliyebaki kwenye kikosi chake atakuwa sawa na anataka kuwaangalia mastaa wake watatu ambao ni Feisal Salum, Farid Mussa na Mukoko Tonombe kwa jinsi gani wanaweza kufanya mabadiliko chanya katika kikosi chake.
“Tunaweza kuangalia matumizi mengine ya Feisal kama tutaona atafaa, lakini tuna Farid nimekaa naye Zanzibar tumefanya vikao kuna mambo nataka abadilike awe na kiwango bora zaidi, wakati mwingine tuna Mukoko ni mchezaji muhimu naye tutamuangalia,” alisema Nabi na kuongeza.
“Siwezi kuweka wazi jinsi gani tutabadilisha mbinu zetu, hayo tutayafanyia kazi huku ndani, lakini wako wengi ambao tunaweza kuangalia jinsi tutakavyowatumia ili tuwe bora zaidi.”
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: