JE, UTAIKUMBUKA HII?? HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KWENYE UZINDUZI WA ALBUM YA WAONA NINI YA KWAYA YA USHARIKA MWAKA 2015
Kushoto ni Msanii/Mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Olexander wa Vioja Mahakamani akisisitiza jambo kanisani
Hapa ni katika kanisa la KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga ambapo leo kumefanyika tamasha la Uzinduzi wa Albamu inayojulikana kwa jina la “Waona Nini” kutoka kwaya ya Usharika ya KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga yenye nyimbo 11,ambapo watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania wamehudhuria uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakiwemo wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na mwenyekiti wa wenyeviti hao Mgana Msindai walikuwepo bila kumsahau Msanii/mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Olexander(Mmasai) wa Vioja Mahakamani.Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw. Philemon Mollel.
Kwaya ya Unjilisti kutoka Arusha pia ilikuwepo katika uzinduzi huo. Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala ndiye aliyeweka wakfu albamu/kanda hiyo ili injili ihubiriwe kote ulimwenguni kwa njia ya uimbaji.
Wakati wa uzinduzi wa Albamu hiyo kulifanyika harambee ya Ununuzi wa CD/Zoezi la kuuza CD ambapo jumla ya shilingi milioni 21,laki5,52 elfu na 500.
Wanakwaya wa kwaya ya Usharika ya KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga wakiimba wimbo wa “Waona Nini” katika kanisa hilo.Albamu ya “Waona Nini”.
Mpiga kinanda wa kwaya ya Usharika ya KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga Martin Masele akifanya yake kanisani
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo
Wanakwaya wakiimba kwa hisia
Ebwana eee,wanacheza na kuimba vizuri sana
Bwana Isaack Luhende ambaye ndiyo mwalimu mkuu wa kwaya hiyo akiimba kanisani wakati wa uzinduzi
Hapo sasa.....!!wanacheza kwa madaha kweli kweli
Wageni waaalikwa wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kanisani
Mwenyekiti wa kwaya ya Usharika ya KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga Abel Katalana akisoma risala kuhusu Albamu ya "Waona Nini" ambapo alisema hadi kukamilika kwake jumla ya shilingi milioni 19,laki 6,elfu 50 na 500.
Mwenyekiti wa kwaya ya Usharika ya KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga Abel Katalana alisema hiyo ni albamu ya 3 tangu kuanzishwa kwa kwaya hiyo ambayo mlezi mkuu ni Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Albamu hiyo ambapo alisema itakuwa chachu ya uinjilishaji injili duniani kote
Wageni waalikwa wakitambulishwa katika kanisa hilo wakati wa uzinduzi huo
Wanakwaya wa kwaya ya Uinjilisti kutoka Arusha mjini waliosindikiza Uzinduzi wa Albam hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kanisani
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala akiweka wakfu albamu hiyo
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Philemon Mollel akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Philemon Mollel akizungumza wakati wa uzinduzi huo,kulia kwake ni msaidizi wa Askofu, mchungaji Trafaina Nkya
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Philemon Mollel akitoa zawadi kwa viongozi mbalimbali wa kwaya hiyo waliofanikisha shughuli ya kukamilisha albamu hiyo,
Kulia ni meneja wa Hifadhi ya Chakula kanda ya kaskazini ndugu Bright Mollel akishikana mkono na Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala
Wanakwaya wa kwaya ya Uinjilisti kutoka Arusha mjini wakiimba
Wanakwaya kutoka Arusha wakiimba kwa hisia
Tunafuatilia kinachoendelea......
Kulia ni mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Olexander wa Vioja Mahakamani.
Tunafuatilia kinachoendelea kanisani....
Kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja,akifuatiwa na mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Olexander wa Vioja Mahakamani.
Kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangole,akifuatiwa na mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM nchini Mgana Msindai ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,kulia kwake ni Meneja wa Hifadhi ya Chakula kanda ya kaskazini ndugu Bright Mollel
Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM nchini Mgana Msindai ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida akizungumza kanisani hapo wakati wa harambee ya kununua CD za albamu ya "Waona Nini"
Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM nchini Mgana Msindai ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida akizungumza kanisani hapo leo
Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM nchini Mgana Msindai ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida akishikana mkono na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Philemon Mollel baada ya kununua CD
Mama Shoo miongoni mwa Ma MC katika tamasha hilo la uzinduzi akisisitiza jambo
Viongozi mbalimbali wa kanisa la KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga wakijiandaa kununua CD
Zoezi la kununua CD linaendelea
Wanafuatilia kinachoendelea kanisani
Kila mtu alikuwa makini kanisani
Kushoto ni Mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Olexander wa Vioja Mahakamani akisisitiza jambo kanisani wakati wa kuuza CD za albamu ya "Waona Nini"
Kushoto ni Mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Olexander wa Vioja Mahakamani akisisitiza jambo kanisani
Waimbaji wa kwaya hiyo wakisikiliza kinachoendelea kanisani
Watoto wakiwa wameshikilia CD baada ya kununua kanisani kwa bei nafuu kabisa
Zoezi kununua CD linaendelea
Meneja wa Hifadhi ya Chakula kanda ya kaskazini ndugu Bright Mollel akizungumza wakati wa kununua CD
Wanakwaya wakifurahia CD zao kununuliwa
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangole akizungumza wakati wa kununua CD
Zoezi la kununua CD linaendelea
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ambaye ni Muislam akizungumza wakati wa kununua CD
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akishikana mkono na mgeni rasmi
Kushoto ni Meneja wa Hifadhi ya Chakula kanda ya kaskazini ndugu Bright Mollel akijiandaa kununua cd
Meneja wa Hifadhi ya Chakula kanda ya kaskazini ndugu Bright Mollel na wageni waalikwa kutoka Arusha wakijiandaa kununua CD
Furaha ilitawala
Uinjilisti kwaya kutoka Arusha wakijiandaa kununua CD
Mchekeshaji kutoka Kenya Olexander akifanya yake kanisani
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangole akiimba kwaya
Uinjilisti kwaya wakiimba kanisani
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala akiwakabidhi CD wanakwaya wa Uinjilisti kutoka Arusha ili wampeleke askofu wa Arusha
Mwanakwaya akionesha CD za "Waona Nini"
Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala akimpa mkono wa shukrani Mgeni rasmi Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Philemon Mollel kwa kushiriki tamasha la Uzinduzi wa albamu ya "Waona Nini" .
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi