KOCHA MPYA WA SIMBA ATOA SHERIA NA MASHARTI MAKALI KWA WACHEZAJI, HITMANA ASHINDWA KUJIZUIA

KOCHA wa Simba,Pablo Franco amewaambia viongozi kwamba ishu ya kwanza kwenye timu ni fiziki kwani amebaini kwamba ipo chini na inahitaji kufanyiwa kazi kwa nguvu.


Katika kuhakikisha hilo amewaambia pia wachezaji kila mmoja afanye programu za ziada za ndani na nje ya uwanja kwa haraka sana ili kwenda na kasi yake.

Lakini katika kutekeleza hilo, wachezaji wawili wamemuelewa fasta wakaamua kujiongeza wenyewe ambao ni Pascal Wawa na Hassan Dilunga.

Wachezaji hao tangu Kocha huyo aanze programu zake wameomnyesha kujituma kwa hali ya juu na kufanya mambo mengi ya ziada. Kocha Thiery Hitimana aliweka wazi hivikaribuni kwamba walikaa na Wawa na akamueleza kwamba hakufanya vizuri kimataifa hivyo atalazimika kukaa benchi ajitathmini upya. Dilunga yeye amekuwa hapati namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Simba mikononi mwa makocha kadhaa.

Mwanaspoti linajua kwamba Pablo tayari ameshakaa na wasaidizi wake, Seleman Matola na Thiery Hitimana na kuwaeleza pia wachezaji kama hawako kambini lazima wakutane kwanza tofauti na utaratibu alioukuta wa watu kupitiliza moja kwa moja mazoezini Bunju.

Katika mazoezi yaliyofanyika chini yake wiki hii inaelezwa amekuwa akisisitiza uharaka wa kila jambo mchezaji anapokuwa uwanjani na hataki mzaha wowote au kumuona mtu anatembea tu.

HITIMANA: JAMAA ANAJUA
Hitimana alisema kikosi chao kwa sasa hakina wachezaji wengi waliokuwa katika timu inayocheza mechi shindani wengi ni wale kutoka katika timu ya vijana.

Hitimana alisema anadhani akipata muda zaidi wa kukaa na Franco ataelewa mambo mengi kutoka kwake haswa wakiwepo na wale wachezaji waliokuwepo katika timu ya taifa wakati huu.

“Kuna vitu vizuri kutoka kwake kwa muda huu mfupi tuliokuwa nae anamalengo makubwa kuona Simba inafanya vitu ambavyo vitakuwa silaha ya kufika mbali na kufikia mafanikio,” alisema Hitimana na kuongeza;

“Wasaidizi wake tupo tayari kumpatia ushirikiano katika falsafa zake na kile ambacho anahitaji katika timu ili kuona malengo ya klabu tunayafikia.”

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.