HII KALI!! SIMBA WATOA MSIMAMO WAO KUHUSU UNUNUAJI WA MECHI ZA LIGI KUU

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amevunja ukimya na kudai klabu yao haifanyi mipango ya nje ya uwanja ili kupata matokeo.

Mangungu ametoa kauli hiyo kwenye mkutano mkuu wa Simba uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Mangungu alianza kwa kufichua kuwa mwaka huu ulikuwa mgumu kwa klabu yao hasa baada ya kuwapoteza watu mahiri ndani ya klabu hiyo.

Alisema kingine ni kuanza ligi vibaya msimu uliopita.

"Msimu huu tumeanza vizuri niweke wazi hili, kuna maneno maneno lakini Simba hatufanyi mipango nje ya uwanja, tunacheza uwanjani na kupata matokeo," amesema Mangungu huku akitania kuwa kuna timu hadi penati inapigwa na watu wanane.

Mangungu pia alizungumzia katiba ya klabu na kubainisha aina za wanachama ambao wapo waliokuwa na kadi za zamani na mpaka sasa hawajapata kadi mpya.

"Pia wanachama wenye kadi mpya lakini hawajaingizwa kwenye kumbukumbu za klabu na wale ambao wamelipia kadi zao na hawajapata, hilo tunalishughulikia.

Alisema kwenye matawi pia wana mkakati kila mkoa uwe na tawi la klabu hiyo linaloeleweka.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.