DODOMA JIJI YAICHAPA PRISONS 2-1 DODOMA

WENYEJI, Dodoma Jiji FC waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mabao ya Dodoma Jiji yalifungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 37 kwa penalti na Emmanuel Martin dakika ya 59, wakati la Prisons limefungwa na Jeremiah Juma dakika ya tatu.

Dodoma Jiji wanafikisha pointi saba baada ya mechi nne na kusogea nafasi ya tatu wakizidiwa pointi mbili na Yanga na Polisi Tanzania ambazo zimecheza mechi tatu kila moja.
Tanzania Prisons inabaki na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.