YANGA YATEMBEZA MKWARA, KUISIMAMISHA NCHI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba unakwenda kufanya jambo kubwa kwenye mchezo wa marudio dhidi ya Rivers United ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Jumapili.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na maumivu ya kunyooshwa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kazi kubwa ambayo wanayo kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya awali ni kupindua meza kibabe ili waweze kusonga mbele.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara ameweka wazi kwamba wanakwenda kwenye mchezo huo kupambana ili kupata matokeo mazuri.

"Tumefanya usajili mzuri na imera hilo ni jambo ambalo ninapenda kukuhakikishia masuala ya ufundi hayo benchi la ufundi wanajua na wanakazi ya kufanya.

Kuhusu mchezo wa Jumapili, Manara amesema:"Hii ndio Yanga na tutakachokwenda kukifanya Afrika itasimama, Insha'Allah'," .

Yanga wanatarajia kukwea pipa Septemba 17 na watarejea Septemba 19 kwa kuwa mchezo wao unatarajiwa kuchezwa Septemba 19 hivyo mchezo ukimalizika wanarejea.

Ni ndege ya kukodi kutoka Tanzania, Air Tanzania itatumiwa na msafara wa wachezaji pamoja na viongozi wa Yanga.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.