MAALIM SEIF AMWANDIKIA BARUA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JAJI MTUNGI
Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF na aliyekuwa mgombea uraisi katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Tanzania visiwani (Zanzibar) kwa tiketi ya UKAWA ndugu Maalim Seif, amemwandikia barua msajili wa vyama vya siasa jaji Francis Mtungi kupinga barua yake iliyoeleza kumtambua Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho.
Katibu mkuu huyu aliwasilisha barua yake kwa msajili wa vyama vya siasa tarehe 27 Septemba, 2016 akieleza kupokea barua yake. Katibu Maalim Seif alieleza kuwa, msajili wa wa vyama vya siasa hana mamlaka ya kutoa sheria kwa chama cha siasa kilichosajiliwa.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi