KUTANA NA JAMBAZI ALIYEIBA FEDHA KWQENYE BENKI 50 KWA USTADI WA HALI YA JUU ZAIDI DUNIANI


Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.

Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber)

Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'!

Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia au kumkamata.

Mbinu, weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio yake yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya kifungo.. Na hii ni historia yake 'kwa kifupi' tu

ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEVU"
Akiwa na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi ambapo alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na alipigwa risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa katika jela ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.

Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo (majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha, ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na fedha.

Baada ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na alichofanya ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo alisomea Uhandisi wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na programu maalum ya jeshi la marekani kwa ajili ya kurecruit vijana walioko chuoni! Baada ya kumaliza Chuo akaenda kutumikia jeshi kwa muda mfupi kituo cha Fort Bragg na akiwa huko akapata mafunzo maalumu ya kijeshi (Special Forces and tactical weapons training)

Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi Carl akarudi Chuo kusoma masters degree ya System Analysis na alipomaliza masters degree akafanya mafunzo ya awali kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika Statistics.

Pia mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo ya kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi (third degree black belt)

Baada ya kufanikiwa kufanya maandalizi yote hayo na kupata kila aina ya mafunzo na uzoefu aliyohitaji ili kuwa 'muhalifu wa daraja la kwanza' sasa ulikuwa ni wakati kwake kupita kila benki kukomba hela na kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakujapata kuwepo na itachukua miaka mingi kutokea muhalifu professional kama yeye Carl 'the Friday night bank robber'.

MAANDALIZI KABLA YA TUKIO.
Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu.

Kwanza kabisa Carl ali scout bank zilizopo katika miji midogo. Baada ya kupata orodha ya benki katika miji kadhaa midogo then Carl aliangalia kati ya bank hizo ni bank gani haziko katikati ya mji (kwa maana kwamba ziko pembezoni/nje ya mji). Kisha Carl aliichagua bank moja wapo kati ya hizo na bank ambayo inakuwa haiko karibu sana na makazi ya watu au iko karibu na msitu basi bank hiyo anaipa kioaumbele katika orodha yake.

Baada ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya tukio lenyewe atakavyolitekeleza... Kwanza kabisa Carl alianza kwa kusoma mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank.. Inaelezwa kuwa Carl angeutembelea msitu huo na kuukagua nukta baada ya nukta, haijalishi ni muda gani angetumia mpaka kumaliza kuukagua!

Inaelezwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu ambapo watu huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la msitu limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu nukta kwa nukta!

Baada ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank husika.. Hapa alitafiti kuhusu 'shifti' zao za kazini, nanj ni teller, nani ni manager na pia kitu kingine cha msingi alijitahidi kuwasoma personality zao.

Baada ya kumaliza kufanya 'tafiti' zake Carl alienda hatua ya pili ya maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa 'makazi na stoo' yake ya muda katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna yoyote ile.. Moja ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata Carl anaeleza Bw. Carr anaeleza kuwa siku ambayo walifanikiwa kugundua na kuliona handani mojawapo ambalo lilichimbbwa na Carl walistaajabu (kumbuka Carl alikuwa na zaidi ya mahandaki 30 sehemu tofauti tofauti za nchi ya marekani)! Inaelezwa kuwa kinachostaajabisha kuhusu mahandaki ya Carl ni jinsi yalivyo chimbwa kiustadi na kujengewa kwa ndani kwa vitofali vidogo vidogo.. Pia handaki lilikuwa linampangilio wa hali ya juu wa kiwango cha kijeshi (military precision). Ndani ya handaki kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka za 'research', kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura (first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu, majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi..

Baada ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika maktaba ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake kwani inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo akifanya 'tafiti' na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize mpango wake na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio lenyewe.

UTEKELEZAJI WA TUKIO.
Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema!

Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'..

Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..

Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka 'harufu' kwenye nyumba zote zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu kutafuta trail ya alikoelekea!

Siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha kutisha usoni ambacho kili-fit sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake na! Pia alivaa manguo mengi ili kuleta muonekano kwamba ni mnene.. Na alikuwa akiingia ndani ya bank alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano wa Kaa (crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda alikuwa na matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi kabisa.. Alivaa kinyago cha kutisha ili kuleta effect ya kuogofya na kuficha tone ya ngozi yake, pia alivaa manguo mengi ili kuficha body size, na alitembea kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha height!! Hii ilimsaidia sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung'amua mtu wanayemtafuta alikuwa wa size gani, height gani au skin color ipi?

KUVAMIA.
Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia..

Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio karibu..

Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni..

Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia kwa dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida anaendesha baisikeli anaondoka! Carl anasema kuwa ataendesha baisikeli kwa muda wa kama dakika ishirini au zaidi mpaka upande wa pili wa msitu ambapo kuna barabara na hapo kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri.. then anawek baisikeli ndani ya gari anaendesha kama raia wa kawaida na kuelekea nyumbani.

Carl anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua 'hela zake'. Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza 'tafiti' kwa ajili ya tukio linalofuata.

KUKAMATWA NA HUKUMU.
Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno! Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani.. Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawqpeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana wanadeal na ishu serious kuliko uwezo wao hivyo wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu kung'amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na Jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.

FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate kumtrack down Carl mpaka wakampata.
Siku Carl anakamatwa alikutwa "ofisini kwake" Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya "tafiti"

Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili lakini mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna ya kuwabaini 'serial criminals', na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!

Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..

Hivyo basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.