ARTETA KUMPA MAJUKUMU AARON
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuwa anaweza kumtumia Aaron Ramsdale kama kipa namba moja wa timu hiyo.
Aaron alifanikiwa kuitumikia Arsenal kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England ambapo timu yake ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norwich City.
Kocha huyo amesema inawezekana pia akaamua kuendelea kumtumia Bernd Leno kwa kuwa atakachokuwa anakiangalia kwa sasa ni kiwango cha mchezaji husika.
Leno amekuwa kipa namba moja kwenye kikosi cha Arsenal kuanzia mwaka 2018 na sasa ndiyo anaonekana kupata mpinzani.
“Huyu ni kipa bora, siyo kwa jinsi anavyodaka tu bali hata jinsi ambavyo amekuwa akielekezana na mabeki wake.
“Nafikiri ni mmoja kati ya makipa bora England na anaweza kuwa kipa namba moja hapa, ishu ya nani anaweza kuwa bora inaanzia mazoezini.
“Mimi nitakuwa namchukua kipa wa kucheza kulingana na jinsi ambavyo watakuwa wakifanya kwenye mazoezi, nafikiri huyu ni mmoja kati ya wale ambao wanaweza kuchukua nafasi hiyo.
“Tuna makipa wawili bora sana, nafikiri tunaweza kufanya vizuri sana msimu huu kama tutaendelea kujituma na kuendelea kupunguza makosa kila siku “,alisema Arteta.
Arsenal wapo kwenye presha kubwa wakiwa wameshapoteza michezo mitatu mfululizo ya mwanzoni mwa msimu huu.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: