HAJI MANARA AFUNGUKA MAZITO, ASEMA SIMBA NA YANGA SIO UADUI....AELEZA KUWA MTOTO WAKE WA KUZAA NI YANGA DAMU

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara, amefunguka kuhusu matusi anayoyapata kutoka kwa mashabiki wa Yanga.

Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Manara amesema anatukanwa sana na mashabiki wa Yanga mpaka imefikia hatua wanamuunganisha kwenye magroup yao ya Whatsapp ya timu yao.

“Ninatukanwa sana, matusi mabaya ya ushamba, na wengine wananiunga hadi kwenye magroup ya whatsapp ya Yanga,” amesema Manara.

“Simba na Yanga sio uadui ni watani wa jadi. Mimi mwanangu mwenyewe wa kumzaa ni Yanga,” ameongeza.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.