WATALII 10 WADAIWA KUTEKWA ARUSHA

Kundi la watalii zaidi ya 10 waliokuwa wakisafiri kutoka jijini Arusha wakielekea kutalii katika hifadhi ya Serengeti wametekwa na watu wasiojulikana na kisha kupigwa na kuporwa Mali mbalimbali.

Watalii hao wanadaiwa kutekwa katika kijiji cha Maloni umbali mchache kutoka eneo la Lake Natron ambako walikuwa wameweka kambi wakijiandaa na safari ya kwenda kutalii wilayani Serengeti.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Devotha James amesema kwamba tukio hilo limetokea saa 12:30 jana jioni watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao waliweka kizuizi barabarani.

Shuhuda huyo amesema kwamba watu hao walizuia magari mawili ya kampuni ya utalii ya Gladness katika barabara hiyo na gari moja kufanikiwa kukwepa kizuizi hicho na kukimbia kurudi bararabara ya Arusha.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo alithibitisha taarifa za tukio hilo na kusema kwamba jeshi lake linaendelea kufuatilia Kwa undani kutokana na eneo lenyewe kutokuwa na mawasiliano mazuri.

Mwananchi

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.