MAMA SAMIA SULUHU AWAFUNDA WANAUME ''MSIPENDE KUWAONA WAKUBWA WENZENU HAWANA LADHA KATIKA TENDO LA NDOA''
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu amewahasa wanaume wote wa Tanzania kutowaona wakubwa wenzao wamechuja katika tendo la ndoa na kuanza kuwataka watoto wadogo ambao ni watoto wao na taifa la kesho.
Akizungumza leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi ambapo pamoja na hilo amesema wapo baadhi ya wanaume ambao wanajua wameshaambukizwa bado wanaendelea kuwaambukiza watoto hao.
“Wanaume msipende kuwaona wakubwa wenzenu wamechuja hawana ladha ile ambayo mngependa kuipata, kwahiyo mna hamia kwa watoto wadogo ndugu zangu huu sio mwendo mzuri hawa ni watoto wetu, hili ni taifa la kesho tukiliteketeza leo, na wengine wanajua wameshaambukizwa na wakubwa wanaushifti kwa watoto wadogo ambao ambao hawawajui, ndugu zangu huu ni uuwaji wa makusudi na Mwenyezi Mungu hatawasamehe katika hili,” amesema Mama Samia.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: