MUGABE AKATAA WITO WA KUJIUZULU URAIS ZIMBABWE

Mugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia)


Rais wa miaka mingi nchini Zimbabwe anaripotiwa kukataa kuondoka madarakanI mara moja licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu.

Mugabe, 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Mugabe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema.

Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani.

Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alisema mapema kuwa kwa manufaa ya watu Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja.Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yake

Jeshi lilichukua hatua baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopiya, na kuashiria kuwa alimpendelea mke wake Grace Mugabe, kuchukua uongozi wa chama cha Zanu-PF na kuwa rais.

Taarifa zinasema kuwa Mugabe ambaye alikuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwak 1980 anakataa kuondoka kwa hiari kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.

Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa Bw. Mugabe anaweza kujaribu kujihakikishia usalama na familia yake kabla ya kuondoka madarakani.

Maafisa wa Zanu PF mapema walikuwa wamesema kuwa Bw. Mugabe atasalia madarakani hadi ufanyika mkutano mkuu wa Chama mwezi Disemba wakati Bw. Mnangagwa atakiongoza chama na hatimaye kuwa raisBw Mugabe alikutana na maafisa katika ikulu ya Harare

 Chanzo-BBC

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.