KATAMBI ATANGAZA MAFANIKIO ALIYOFANYA SHINYANGA MJINI, HAPI AKEMEA MASHABIKI FEKI NA MADALALI WA KISIASA

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Wajumbe Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakionesha picha ya Rais Samia Suluhu Hassan

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Chama Mapinduzi (CCM) Ally Hapi akizungumza leo Januari 24,2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini  ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Na Marco Maduhu & Kadama Malunde - Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka 2020/2024 na kuthibitisha kwamba amefanikiwa kuitekeleza kwa asilimia 100 akitumia kauli mbiu yake ya 'Shinyanga Yetu, Maendeleo Jukumu langu'. 

Taarifa hiyo amewasilisha  leo Ijumaa Januari 24,2025 mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM jimbo la Shinyanga Mjini, ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi.

Utekelezaji wa Ilani ya CCM

Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, ameeleza hatua mbalimbali alizochukua katika kipindi cha miaka minne cha uongozi wake.

 Ameweka bayana mafanikio katika sekta mbalimbali kama vile elimu, miundombinu, afya, maji, na huduma za kijamii.

Elimu

Kwa upande wa elimu, Katambi amesema kuwa alipofika katika jimbo hili alikuta upungufu wa madarasa manne, lakini alifanikiwa kujenga shule mpya tisa (5 za msingi na 4 za sekondari).

 Aidha, amefanikisha kuanzishwa kwa tawi la Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na upanuzi wa Chuo Kikuu cha Moshi (KICoB) tawi la Kizumbi.

Mhe. Patrobas Paschal Katambi

Miundombinu

Katambi ameeleza mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli na uboreshaji wa barabara na madaraja yaliyo korofi kama vile la Uzogole, Iwelyangula, na Kitangili. 

Pia, ameomba serikali kusukuma mbele mradi wa barabara ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza. Vilevile, ameelezea mafanikio ya ujenzi wa stendi mpya na masoko mbalimbali.

Afya

Katambi amebainisha kwamba ameboresha miundombinu ya afya, ikiwa ni pamoja na kituo cha afya cha Kambarage, hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na Hospitali ya Rufaa. Pia ametoa ambulensi zaidi ya sita kwa ajili ya kuboresha huduma za usafiri kwa wagonjwa.

Wajumbe Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakionesha picha ya Rais Samia Suluhu Hassan

Maji

Kwa upande wa maji, amesema kwamba wamefanikiwa kuongeza mtandao wa maji kwa wananchi na kusambaza huduma hii katika maeneo kama Bugwandege, Masekelo na Mwamasheke. 

Pia ameeleza kuwa amepokea shilingi bilioni 195 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika jimbo hilo na mradi utaanza mwaka 2024/2025.

Mikopo na Uchumi

Katambi amesisitiza kuwa ametoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi mbalimbali vya boda boda, bajaji, wanawake, na watu wenye ulemavu, huku akitaja pia mikopo mingine aliyotolewa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha, aliongeza kuwa amefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi milioni 800 hadi shilingi bilioni 5.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Nishati Safi ya Kupikia

Katambi pia ameelezea hatua alizochukua katika kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kugawa mitungi ya gesi 1,780 kwa wananchi.

Michezo na Utamaduni

Katika kuunga mkono michezo, Katambi amesema amekuwepo na ufadhili wa ligi mbalimbali za michezo na kutoa zawadi nono kwa washindi, hadi shilingi milioni 6.

Ujenzi wa Ofisi za Chama

Kwa upande wa maendeleo ya chama, Katambi amesema ameweza kujenga ofisi za chama katika maeneo mbalimbali ya jimbo, ikiwa ni pamoja na ofisi ya Ibadakuli sh.milioni 54 pamoja na Chibe yenye thamani ya sh.milioni 48.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, amempongeza Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo, na kusema kuwa hatua hiyo inajenga imani kubwa kwa wananchi na kuiwezesha CCM kupata ushindi katika uchaguzi Mkuu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi

"Utekelezaji wa Ilani ndiyo kazi ya msingi na uhai wa Chama," amesema Hapi, akisisitiza kwamba kazi nzuri ya utekelezaji wa ahadi za chama ndio itakayowapa wabunge na madiwani ushindi katika uchaguzi ujao. Alisema kuwa, ni muhimu kwa viongozi kuendelea kutimiza ahadi zao kwa wananchi na kuepuka kukatishwa tamaa na watu wanaowania nafasi zao.

Nidhamu ya Chama na Tahadhari kwa Madalali wa Kisiasa

Aidha, Hapi amewataka viongozi wa CCM, wakiwemo wabunge na madiwani, kuendelea kufanya kazi kwa bidii, huku akisisitiza kwa nguvu zote kwamba kampeni kabla ya wakati hazifai. 

Ameonya dhidi ya Mashabiki feki na madalali wa kisiasa, akisema kuwa ni lazima waangalie kwa umakini ili kuepuka kuharibiwa na wanasiasa wanaotumia mbinu za kijanja ili kuvuruga chama.

"Watia nia jihadharini na wapambe feki. Siasa ni kama ulevi—mtauza kila kitu na kubaki weupe," ameonya Hapi, akitahadharisha dhidi ya wanasiasa wanaoweza kuchafua majina na maadili ya chama kwa kupiga kampeni kabla ya wakati.

Uchaguzi wa Kisayansi na Usimamizi wa Nidhamu

Hapi amesisitiza kwamba uchaguzi wa mwaka huu ni wa kujipanga, na kila mtu atajulikana kwa kazi alizozifanya kwa wananchi. 

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameshachana mikeka ya wale wanaopanga safu kabla ya muda, huku pia Takukuru ikitakiwa kuwa macho kwenye uchaguzi wa ndani ya chama kuhusu wabunge na madiwani watakaosimama kwa niaba ya CCM.

"Viongozi wanapaswa kuelezea utekelezaji wa Ilani kwa wananchi ili kupata ushindi wa kishindo," ameongeza Hapi, akisema kuwa siasa za kisayansi, kujenga hoja, na utekelezaji wa ahadi ndio vitakavyowawezesha CCM kushinda.

Miongozo ya CCM

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo, amempongeza Katambi kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ,huku akimtaka apige kazi na kuonya watu ambao wamekuwa wakivunja kanuni na maadili ya Chama hicho na kuanza kufanya kampeni za kugombea Ubunge kabla ya wakati.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo.

“Acheni Mbunge ambaye bado yupo Madarakani afanye kazi, msipige Kampeni kabla ya wakati hata Mwenyekiti wetu Taifa ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan ameonya hilo na mimi nitaendelea kusimamia nidhamu ya Chama,”amesema Odilia.

Amewataka wanaCCM waendelee kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepuka migawanyiko.

Misaada ya Kijamii na Uungaji Mkono wa Mbunge Katambi

Katika mkutano huo, Mbunge Katambi amekabidhi kiti mwendo kwa mtoto mwenye ulemavu, Delfina Mashaka, kikiwa kimekabidhiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi.

 Vilevile, amekabidhi Spika 4 na Microphone 4 kwa uongozi wa Stendi ya Mabasi ya Mkoani Shinyanga, akionyesha kuendelea kuunga mkono maendeleo ya kijamii na huduma bora kwa wananchi.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Chama Mapinduzi (CCM) Ally Hapi akizungumza leo Januari 24,2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini  ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwa ajili ya kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Chama Mapinduzi (CCM) Ally Hapi akizungumza leo Januari 24,2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini  ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwa ajili ya kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwa ajili ya kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini
Wajumbe Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakionesha picha ya Rais Samia Suluhu Hassan
Wajumbe Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa ukumbini
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Wajumbe Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakionesha picha ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi
Wajumbe Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakionesha picha ya Rais Samia Suluhu Hassan
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi (wa tatu kulia) akikabidhi kiti mwendo kwa mtoto mwenye mahitaj maalum kilichotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi (wa nne kulia) akikabidhi fedha kwa mtoto mwenye mahitaj maalum kilichotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akizungumza wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024
Wajumbe Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa ukumbini

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.