Breaking News: ALIYEKUWA MUME WA IRENE UWOYA NDIKUMANA AFARIKI DUNIA

Msiba mkubwa kwa Taifa la Rwanda! Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia usiku wa kuamukia leo.

Kataut beki wa zamani wa Rayon Sports na mume wa muigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amefariki dunia baada ya kuugua ghafla.

Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza Kataut alikuwa mazoezini jana asubuhi.

Wakati anapoteza maisha, Kataut alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.

Mara ya mwisho, Kataut aliichezea Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.

Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.