DKT. LOUIS SHIKA ASIMULIA KWA UNDANI MWANZO HADI MWISHO KILICHOSABABISHA AKAWEKWA NDANI
Baada ya kuachiwa kwa dhamana na jeshi la polisi,mshindi wa mnada wa uuzaji wa nyumba za Lugumi, dokta Louis Shika na kuelekea nyumbani kwake, Dokta huyo amefunguka mambo mengi yaliyojiri katika kituo cha polisi, jinsi mnada wa ununuzi wa nyumba za Lugumi ulivyokuwa umepangwa na kwamba kilichosababisha ni kutokuelewana.
Akijitambulisha alisema "Mimi ni dk Louis Shika Kiti ni rais wa kampuni ya kimataifa inayoita LENSFORT yenye makao makuu yake Moscow Urusi na sasa hivi nafikiri umefika muda tunaingia Afrika na tunaanza na Tanzania ambako ndiko nimetoka"
Alipoulizwa nini kilichosababisha mpaka akawekwa ndani alisema "Tatizo nafikiri ni kutoelewana, YONO(kampuni ya udalali) walisemaaa kuwa tarehe 9/11/2017 saa nne na nusu wataanza mnada wa majumba ya Lugumi na wataanza na Mbweni na kumalizia Upanga. Hiyo taarifa walinitumia ujumbe kama walivyokuwa wameniahidi kuwa watanitumia taarifa wakiwa tayari. Taarifa hiyo baada ya kuipata mimi nilifika mapema sana saa mbili asubuhi ambapo wao walifika wakiwa wamechelewa sana kwenye kama saa tano kuelekea saa sita" alieleza
"Kilicholeta kutokuelewana ni pale ambapo yule mama aliyekuwa anatangaza alianza kusema atakayeshinda atalipa 25% hapa hapa na mimi hilo nikalisikia na baadae akauliza kama kuna mtu ana swali, mimi nilinyanyua mkono nikamwambia kuwa mimi hela kama hizo sitembei nazo mfukoni na yeye akanijibu kuwa nisiwe na hofu kwani nitafanya transfer ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine. Basi baada ya hapo mimi nikarelax kwa sababu uwezo wa kutransfer fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine ninao hivyo nikaona tuendelee na mnada. Ukamalizika mnada wa nyumba ya kwanza ambayo iliuzwa milioni 900, na nyumba ya pili Tsh. bilioni1.2 na baadae tukaja nyumba ya Upanga nayo ikauzwa Tsh. bilioni 1.2" alisimulia
"Sasa basi, ukaja ugomvi yale maneno niliyokuwa nimeambiwa nitatransfa likaja neno jingine la kwamba hiyo 25% lazima niilipe leo leo hii wakati neno hili halikutajwa huko Mbweni. Na kama neno la leo leo hii wangelisema mapema nami ningekuwa nimejitoa mapema kabisa, lakini lilipoongezeka neno la leo leo hii basi nikajikuta nimetumbukia na kuingia ambako sio kwenyewe maana mimi hela yangu ipo nje ya nchi hii mpaka niiitishe na nilikuwa nimeshaanza process kuitisha fedha hiyo ili niipate sema tu walini wahi hiyo tarehe 9/11 hela ilikuwa bado haijaingia Tanzania. Huwezi ukaanza process ya kuitisha hela siku hiyo hiyo na ukaipata siku hiyo hiyo au nchi yako unayoitaka, hata kwa njia ya haraka zaidi ya online huwezi ukaipata kwa siku moja tu lazima iwe baada ya siku moja au kutegemea na wingi wa hela iliyoingia lazima Benki iliyoipokea itoe taarifa BOT ili kuona kama fedha hiyo ni halali au sio halali." Alisema dokta Louis"
Siku ile iliyoleta utata huu wa kwamba sina fedha ya siku hiyo hiyo ingawaje nilikuwa na hela nje ya nchi na tayari nilikuwa nimeshaanza kuiitisha tulipoangalia kwenye mtandao nilikuta taarifa inasema kwamba tumekuandikia cheki na tunaituma kwa Kulya na baada ya masa 48 itakuwa imeingia Tanzania na kule mwishoni wakaandika PENDING. Sasa neno PENDING likanipa wasiwasi nami nikawaandikia ujumbe kuwa wameandika neno PENDING wanamaanisha nini?" Baadae walikuja kujibu mimi nikiwa nimeshawekwa ndani tayari sikuliona walikuwa wamejibu nini"
"Jumamosi saa kumi jioni yale masaa 48 waliyokuwa wametoa nikaona yanaisha nami nikiwa bado nimo ndani, wakashauri pale kituo cha Polisi kuwa tuiangalie ile fedha kama tayari imeshaingia Nchini Tanzania na tulipoangalia tukakuta wamejibu kuwa ile fedha hawawezi kuituma kuja huko mpaka niilipie bima. Nikaona kuwa wako sawa ingawaje mimi nilikuwa nimewaomba mapema wakati nawalipa ile fedha nyingine" aliendelea
Kuhusu kuwa na mahusianao na mmiliki wa maghorofa hayo Lugumi, dokta huyo alisema kuwa hajuani na Lugumi na wala hajawahi kuonana nae " Haya ya kuwa na mahusiano na Lugumi yalikuja palepale kwenye mnada niliyasikia pale waliponiuliza kuwa mimi ni kabila gani nami nikajibu kuwa ni msukuma na walipoona u mimi ni msukuma wakajiridhisha na kusema kuw mimi nimetumwa na Lugumi ili niharibu mnada huu kumbe hata haihusianai kabisa"
Dokta Lous Shika alishikiliwa na jeshi la polisi tangu tarehe 9/11/2017 baada ya kushindwa kulipa 25% ya malipo ya nyumba za Lugumi zilizopigwa mnada na kampuni ya Yono na jana aliachiwa kwa jeshi la polisi kwa dhamana
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: