ANGALIA PICHA ZA BILIONEA WA NYUMBA ZA LUGUMI (DOKT. LOUIS) ALIVYOPANDA DALDALA BAADA YA KUACHIWA NA POLISI KWA DHAMANA

Bilionea' wa nyumba za Lugumi, Dk Louis Shika jana aliachiwa na kwenda kupanda daladala kuelekea nyumbani huku akisema mpango wake wa kununua nyumba za Lugumi uko palepale.

Baada ya kuachiwa na polisi jana Jumanne jioni alisema kwamba bado mpango wake wa kununua nyumba hizo uko palepale.

Alisema anachosubiri sasa ni fedha kuingizwa kwenye akaunti yake na kulipa asilimia 25 anayodaiwa.

"Siku nikipeleka fedha nataka Yono na TRA waite waandishi wa habari waone na wautangazie umma," alisema.

Alisema vyombo vya habari vimetoa taarifa zake lakini vitaumbuka siku akienda kupeleka fedha hizo.

Aliendelea kusisitiza kwamba nyumba hizo zinahitajiwa na kampuni yake ambayo hakuitaja.

Njiani wakati akielekea kwenye kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja, Dk Shika alikuwa kivutio kwa watu aliokuwa akipishana nao.

Alipopanda daladala la Tabata Mawenzi, kondakta alimkaribisha kwa kumweleza karibu mzee Shika.

Kauli hiyo iliwaamsha abiria ambao walikuwa na hamu ya kumwona.

Dk Shika alipanda daladala na kusimama huku akionyesha tabasamu lisiloisha.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.