KOCHA MKONGWE TANZANIA ASEMA YANGA KWA DANTE WAMEPATA KIFAA

By Masoud Masasi

Mwanza. Kocha John Tegete amesifu kiwango cha juu alichoonyesha beki wa Yanga, Andrew Vicent “Dante” katika michezo ya Ligi Kuu Bara.
Tegete alisema amekuwa akimfuatilia beki huyo tangu alipokuwa Mtibwa Sugar kubaini kuwa ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee hapa nchini.
Alisema bado mashabiki wa Yanga hawajamuelewa Dante kwa kuwa ni mchezaji mkimya awapo uwanjani, lakini amekuwa msaada mkubwa kwa timu yao.
Kocha huyo alisema sifa kubwa ya mchezaji huyo ni nidhamu yake hawapo uwanjani ambayo imekuwa ikimsaidia sana kucheza mechi kwa kiwango kikubwa na kuisaidie timu yake.
“Mchezaji mzuri ni nidhamu hivi ushawahi kumwona Dante ametaka kupigana uwanja hata ukimkera vipi hawezi kukasirika hivi ndivyo mabeki wanavyotakiwa kuwa,” alisema Tegete.
Mzee Tegete alisema pia uchapaji kazi wake akiwa uwanjani ndio jambo ambalo linamvutia yeye kwani anapenda mchezaji anayejituma kila wakati

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.