JE UNAJUA KITU WANACHOJIVUNIA YANGA KUELEKE MECHI DHIDI YA WATANI WAO JUMAMOSI HII
Klabu bingwa nchini Yanga ambayo jana imeingia jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya Maandalizi ya Mechi dhidi ya Simba Jumamosi Oktoba 28 inajivunia kutokuwa na Majeruhi hata mmoja kuelekea mchezo huo.
Taarifa kutoka Kikosi cha Yanga kilichokuwa Kanda ya ziwa ni kwamba hakuna mchezaji mwenye Matatizo yeyote Kiafya wakati wachezaji ambao hawakuwa fiti na Kulazimika Kubaki Dar nao inaelezwa kuwa wako fiti kabisa kuwakabili Simba.
Wachezaji ambao walibakia Dar ni Kiungo Thaban Kamusoko Na Washambuliaji Donald Ngoma na Amis Joslyn Tambwe ambao wamekuwa wakifanya mazoezi kama kawaida chini ya Uangalizi wa Daktari.
Leo wachezaji Kamusoko, Ngoma na Tambwe wataungana na wenzao kwa ajili ya kambi ambayo mpaka sasa haijajulikana itakuwa wapi.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi