HABARI MPYA MBILI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KUTOKA KLABU YA SIMBA

Klabu ya Simba jana imetua salama visiwa vya Karafuu Zanzibar na kuanza mazoezi yake kujiwinda dhidi ya Yanga October 28 uwanja wa Uhuru, Kulingana na Mratibu wa klabu ya Simba Suleiman Abbas ameliambia gazeti hili kuwa Kikosi kipo katika hali nzuri kabisa.

Wachezaji wangapi wapo katika Kikosi cha Zanzibar na wangapi hawapo?
Suleiman Abbas amesema kikosi kilichoenda Zanzibar kinawachezaji 24 huku wachezaji watatu (3) pekee wakiwa hawapo kwenye msafara huo wa Zanzibar, wachezaji ambao hawapo kwenye msafara huo ni Golikipa Said Mohammed " Nduda " , beki wa Pembeni Shomari Kapombe na Beki wa Kati Salim Mbonde.

Je Simba Itacheza mchezo wa Kirafiki ikiwa Zanzibar?
Suleiman Abbas ameliambia gazeti hili kuwa Suala la Simba kucheza au kutocheza mchezo wa Kirafiki ni suala la mwalimu na benchi lake la Ufundi kama wakihitaji wao wako tayari kuwatafutia mechi ya kirafiki na kwao siyo Tatizo kabisa na wanaamini watapata kirahisi maana Zanzibar ni kama Nyumbani.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.