KOCHA WA YANGA ACHARUKA...KUELEKEA MECHI NA SIMBA, AJA NA GIA MATATA
Licha ya Yanga kupata Ushindi wa bao 4 kwa 0 jana dhidi ya Stand United na tofauti kidogo na Utaratibu wa mwalimu George Lwandamina ambapo amekuwa akitoa mapumziko mafupi mara baada ya Mechi mara nyingi wachezaji wakiachwa wapumzike siku moja lakini safari hii ameendelea na Mazoezi hata baada ya mchezo dhidi ya Stand tena safari Hiii timu ikipiga mazoezi asubuhi na Jioni ya siku ya leo.
Yanga inatarajiwa kuondoka Kesho mjini Shinyanga kwa usafiri wa basi kurejea Dar Es Salaam ambapo Kulingana na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Dismas Ten amesema wakifika Dar ndiyo watasema Kambi yao wataiweka wapi kuelekea mechi dhidi ya Simba Jumamosi October 28, 2017.
Yanga kwa mara ya kwanza jana msomaji wa kwataunit.com Ilipata ushindi mkubwa zaidi msimu huu wa magoli 4 kwa 0 magoli yakifungwa na Ibrahim Ajib akiingia kambani mara 2, Chirwa na Buswita wakifunga bao moja kila Mmoja. Kumbuka Kulike Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi