ZITTO AAMUA KUMSHAURI MAKUBWA WAZIRI MKUU
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto kabwe amshauri hivi Waziri mkuu Kassim Majaliwa
"Jana (Juzi) Waziri Mkuu alionyesha hasira kubwa kuhusu vifungashio vya kampuni ya Minjingu kuonyesha kuwa mbolea ile imetengenezwa Nairobi Mtaa wa Mombasa.
Moja, kifungashio kuwa na jina la mnunuzi ni jambo la kawaida katika biashara hususan mnunuzi anapotaka kudhibiti wizi. Utaona vifungashio vile ni vya Serikali za Majimbo huko Kenya na mbolea ni ya ruzuku. Hata hivyo; hoja muhimu;
Pili, Minjingu hawana kiwanda Nairobi. Ukitazama mifuko ile ni zaidi ya ' branding ' bali mbolea ile ikiwa Kenya itaonekana imezalishwa huko na hapo kuna hoja kubwa mno ya kodi.
Waziri Mkuu amewataka Minjingu kuomba radhi kwa Rais. Nadhani Serikali ifanye uchunguzi kwa kutumia wataalamu wa kodi za kimataifa ( international taxation experts ). Nashauri Waziri Mkuu ahitaji maelezo ya kina kutoka Minjingu kuhusu soko lao la Kenya na aagize International Tax Unit ya TRA ilitazame jambo Hilo. Kwa uzoefu wangu mdogo na nikiwa mmoja wa waanzilishi wa International Tax Unit nchini kwetu ninahisi kuna suala la ukwepaji kodi katika jambo hili. Waziri Mkuu achukue hatua zaidi ya agizo la msamaha. Uchunguzi ufanyike"
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi