Shilole awachana wanaolalamika hali ngumu
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Shilole
Msanii wa muziki wa bongo fleva Zuhena Mohammed alimaarufu kama Shilole amefunguka na kuwapa neno baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakilalamika juu ya hali ngumu ya maisha huku wengi wao wakiitupia lawama Serikali ya awamu ya tanoShilole kupitia mtandao wake wa Instgram amesema amewachana baadhi ya vijana hao na kusema wamekuwa wakilalamika kuwa kuna hali ngumu ya maisha au pesa haipatikani ikiwa wao wenyewe hawahitaji kujishughulisha wamebaki kukaa vijiweni pasipo kuhangaika kutafuta mishe za hapa na pale za kuingiza kipato.
"Unalalamika hali ngumu huku umekaa" aliandika Shilole
Baadhi ya mashabiki wa Shilole wamemuunga mkono kutokana na kauli yake hiyo huku wengine pia wakionyesha kutokubaliana naye wakiendelea kusema kweli maisha ya sasa ni magumu na mishe hakuna.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi