Tani 25 za samaki zakamatwa huko Mbeya
Zaidi ya Tani 25 za Samaki kutoka nchini China ambazo zimepitia bandari ya Dar es salaam, zikisafirishwa kuelekea nchini Zambia zimekamatwa jijini Mbeya zikishushwa kwa ajili ya matumizi ya ndani kinyume cha sheria, na kuikosesha serikali kodi ya zaidi ya shilingi milioni 14, lakini pia ikihofiwa kuhatarisha afya za walaji kwa kuwa samaki hao hawajathibitishwa ubora wakeSamaki hao wamekamatwa majira ya alfajiri Jijini Mbeya ambapo wanadaiwa kusafirishwa kutoka bandari ya Dar es salaam na lori lenye namba za usajili T 343 AWZ na baada ya kufika Jijini Mbeya wameanza kushushwa na kupakiwa kwenye magari mengine madogo madogo kwa ajili ya kupelekwa kwenye duka la mfanyabiashara maarufu wa Samaki jijini Mbeya Joseph Mushi.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa TFDA Rondey Arananga anasema Samaki hao hawajapimwa ubora na mamlaka hiyo hivyo hawawezi kuruhusiwa kutumika hapa nchini, wakati huo Mwakilishi wa Idara ya Uvuvi kutoka kituo cha Tunduma akidai ufungashaji wa samaki hao pia wanatia shaka.
Magari matatu yanayohusishwa na kukamatwa kwa samaki hao yanashikiliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mbeya wakati huo madereva wake na mmiliki wa samaki wakishikiliwa na jeshi la polisi .
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi