KLABU YA YANGA YAMTAMBULISHA KOCHA MSAIDIZI


Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, wamemtambulisha Simo Dladla kutoka Afrika Kusini kama kocha msaidizi kuelekea msimu mpya.

Dladla ni kocha mwenye Leseni ya CAF A, akiwa na uzoefu wa kufundisha katika soka la Afrika Kusini. Kabla ya kujiunga na Yanga, alikuwa kocha msaidizi wa AmaZulu FC, huku akiwahi kuwa kocha mkuu wa Durban City FC (zamani Maritzburg United), baada ya kupandishwa kutoka nafasi ya kocha msaidizi.

Anajulikana kwa kupendelea mfumo wa 4-3-3, unaosisitiza umiliki wa mpira, presha ya juu (high pressing) na kuwapa nafasi wachezaji vijana kuonyesha uwezo wao.

Ujio wa Dladla unatarajiwa kuongeza nguvu katika benchi la ufundi la Yanga kutokana na uzoefu wake wa kufanya kazi katika moja ya ligi zenye ushindani mkubwa barani Afrika.

Mashabiki wa Wananchi sasa watakuwa na matarajio makubwa kuona mchango wake katika safari ya Yanga ya kutetea mataji ya ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa

Post a Comment

0 Comments