
Mwanafunzi wa kike wa darasa la nne kutoka Shule moja ya Msingi iliyopo eneo la Homa bay Nchini kenya mwenye umri wa miaka 10 amelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Homa bay Nchini humo baada ya kushambuliwa na Wanafunzi wenzake kwa kuwaandika kwenye orodha ya wapiga kelele darasani.
Msichana huyo aliyekuwa kiranja wa darasa aliandika majina ya Wanafunzi waliokuwa wakifanya fujo, jambo lililowafanya Walimu kuwaadhibu, hasira za waliotajwa ziliwapelekea kumvamia na kumpiga vibaya hali iliyosababisha kupooza kwa miguu yake yote miwili.
Kwa mujibu wa the Citizen Kenya Madaktari wanasema wanaendelea kumfanyia uchunguzi na matibabu, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea kubaini Wahusika wa shambulio hilo.
Chanzo: CitizenTV