PAMBA JINI YA MWANZA YAPATA AJALI DODOMA


Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, klabu ya mpira wa miguu ya Pamba Jiji imetoa taarifa kuwa wachezaji wa klabu hiyo wamepata ajali mkoani Dodoma wakiwa safarini kuelekea mkoani Morogoro leo Machi 09, 2025.

“Leo majira ya saa 11:00 alfajiri kikosi chetu kilichokuwa safarini kutoka Bukoba mkoani Kagera kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wetu wa Kombe la CRDB

Federation Cup tarehe 11, Machi 2025 dhidi ya Kiluvya United, kimepata ajali ya gari Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma”. imeeleza taarifa hiyo

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, chanzo cha ajali hiyo ni basi lililowabeba wachezaji hao kugongana na lori la kampuni ya Mwanza Huduma na kusababisha mshtuko kwa baadhi ya wachezaji.

“Taarifa za kiusalama zinaendelea, na tutaendelea kuwajuza kitakochokuwa kinaendelea". imeeleza taarifa hiyo

Post a Comment

Previous Post Next Post