MOHAMMED DOUMBIA NI MSHAMBULIAJI MZURI SANA!




Ikiwa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2026/2027 imeanza rasmi jana huku mshambuliaji wa klabu ya Simba Mohamed Doumbia raia wa Mali akishutumiwa na wadau wengi wa soka nchini kama si mshambuliaji mzuri kutokana na mechi alizocheza kutokuonyesha makali kama wengi walivyotarajia hususani kwenye mechi ya dabi ya Kariakoo ya ngao ya jamii kule Zanzibar iliyopigwa tarehe 12/08/2026

Kwa mtazamo wangu, nikimuangalia Doumbia naona kama ni mshambuliaji mzuri tu kwa mechi za ndani kama ligi kuu na FA na kwa hizi mechi huyu jamaa atafunga sana.

Kwa level ya timu zetu za ligi kuu, kama atacheza msimu mzima atafunga magoli 10+

Tatizo kwake ni pale anapokutana na mechi ngumu kama mechi dhidi ya Yanga, Azam au mechi za CAF CC. Mechi hizo kwake ndio zinaweza kuwa ngumu. Ila Doumbia atafunga sana, wanachama na mashabiki wa simba wampe muda tu

Klabu ya Simba kesho watashuka dimbani kukipiga dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera


Isaac Masengwa

Post a Comment

0 Comments