TANESCO, POLISI KAHAMA WAKUTANA KUDHIBITI HUJUMA ZA MIUNDOMBINU YA UMEME

Kaimu Mkuu wa Polisi Kahama (OCD), SP Flora Nangawe, akizungumza katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti hujuma na kulinda miundombinu ya umeme. Picha na Kadama MalundeMeneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Peter Kanuti Magari, akizungumza Agosti 12,2026 katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti hujuma na kulinda miundombinu ya umeme.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Peter Kanuti Magari, akizungumza Agosti 12,2026 katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti hujuma na kulinda miundombinu ya umeme.

Na Kadama Malunde - Kahama

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Kahama limeimarisha ushirikiano na Jeshi la Polisi kwa kuwakutanisha Maafisa wa Polisi kutoka kata 20 za Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, katika kikao maalum cha kujadili namna ya kuzuia na kudhibiti hujuma dhidi ya miundombinu ya umeme.

Kikao hicho kilichofanyika Agosti 12, 2026, kimejikita katika kuimarisha ulinzi wa miundombinu ya TANESCO, ikiwemo transfoma, nyaya za umeme na mita, pamoja na kuboresha ushirikiano kati ya Shirika, Jeshi la Polisi na wananchi katika kutoa taarifa za uhalifu.

Akifungua kikao hicho, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Peter Kanuti Magari, amesema ushirikiano na Jeshi la Polisi ni muhimu katika kujenga mfumo shirikishi wa ulinzi wa miundombinu ya umeme na kukabiliana na vitendo vya hujuma.

“Tunafanya kikao na wenzetu wa kitengo cha usalama TANESCO na askari kata ili kujenga ulinzi jumuishi wa miundombinu ya TANESCO. Shirika limeona ni vizuri kushirikiana na Polisi ili tuwe na uelewa wa pamoja kuhusu miundombinu ya umeme kwa sababu wote tunajenga nyumba moja,” amesema.
Ameeleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kuharibu transfoma, kuiba nyaya za umeme, kuhamisha mita na kufanya vitendo vingine vinavyohatarisha miundombinu ya umeme na huduma kwa wananchi.

Mhandisi Magari ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana kwa karibu na TANESCO katika doria, ufuatiliaji na uchukuaji wa hatua dhidi ya wahujumu, huku akiwataka wananchi kuwa sehemu ya ulinzi kwa kutoa taarifa mapema kuhusu vitendo vya uhalifu.

Amesema TANESCO inaendelea kulithamini Jeshi la Polisi kwa mchango wake katika kulinda miundombinu ya umeme, ikiwemo kudhibiti watu wanaojihusisha na matumizi au uuzaji wa vifaa vya umeme kwa njia za kifisadi.

Kwa upande wake, Afisa Usalama Mkuu Msaidizi wa Uzuiaji TANESCO, Shami Yusuph Dunia, amesema ushirikiano huo utasaidia kuimarisha ulinzi wa miundombinu ya Shirika na kupunguza vitendo vya uharibifu.
Afisa Usalama Mkuu Msaidizi wa Uzuiaji TANESCO, Shami Yusuph Dunia.

Amesema Polisi ni mdau muhimu wa TANESCO katika nyanja mbalimbali za ulinzi na usalama, akibainisha kuwa kikao hicho pia kimekuwa fursa ya kubadilishana uzoefu na kujenga mshikamano kati ya taasisi hizo.

“Madhumuni ya kikao hiki ni kujenga mshikamano na ushirikiano ili kuhakikisha miundombinu yetu inakuwa salama muda wote. Tunaamini kwa kikao hiki mtakuwa mabalozi pia kwa wengine ambao hawajafika kwenye kikao, mtawapa elimu hii na kuifikisha kwa wananchi,” amesema Dunia.

Amesema maafisa hao wamejengewa uwezo na kupata uelewa mpana kuhusu namna ya kutambua, kuzuia na kutoa taarifa kuhusu vitendo vinavyoweza kuhatarisha miundombinu ya umeme.
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Katavi, Abeid Hamad Abeid.

Akitoa mada kuhusu hujuma dhidi ya miundombinu ya TANESCO, Afisa Usalama Mkoa wa Katavi, Abeid Hamad Abeid, amesema miongoni mwa changamoto zinazokabili miundombinu ya umeme ni wizi wa nyaya za umeme.

Amesema eneo la Kahama ni miongoni mwa maeneo yanayokabili changamoto hiyo kwa kiwango kikubwa ndani ya Mkoa wa Shinyanga, hali inayohitaji ushirikiano wa karibu kati ya TANESCO, Polisi na wananchi.

Ameeleza kuwa uharibifu na wizi wa miundombinu ya umeme unaweza kusababisha kukatika kwa huduma, hasara kwa Shirika na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Frank Njavike.

Naye Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Frank Njavike, ametoa wasilisho kuhusu mfumo wa Informer Reward pamoja na Whistle Blower Policy, unaolenga kuhamasisha wananchi na wadau kutoa taarifa kuhusu vitendo vya hujuma dhidi ya miundombinu ya umeme.

Amesisitiza umuhimu wa taarifa za wananchi katika kusaidia TANESCO na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua mapema dhidi ya wahalifu.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Polisi, Kaimu Mkuu wa Polisi Kahama (OCD), SP Flora Nangawe, SP Flora Nangawe, amelishukuru TANESCO kwa kuwashirikisha Polisi katika mkutano huo, akisema elimu iliyotolewa itawasaidia maafisa wa Polisi kufikisha ujumbe kwa wananchi katika maeneo mbalimbali.
Kaimu Mkuu wa Polisi Kahama (OCD), SP Flora Nangawe.

“Tunashukuru kwa ushirikishwaji huu, tunawashukuru kwa kututambua kama wadau wa TANESCO. Tutahakikisha tunawafikia wananchi kwenye maeneo ya ndani ndani,” amesema SP Nangawe.

Amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na TANESCO katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya umeme unaimarishwa na taarifa za uhalifu zinashughulikiwa kwa wakati.
Mbali na suala la ulinzi wa miundombinu, washiriki wa kikao hicho pia wamepatiwa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi iliyotolewa na Maafisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Robert Msemo na Emma Nyaki.

Maafisa hao wamewahamasisha wananchi kutumia nishati safi kwa kuwa ni salama, rahisi kutumia na yenye gharama nafuu, huku wakisisitiza umuhimu wake katika utunzaji wa mazingira.

Wamezitaja pia smart cookers kuwa miongoni mwa teknolojia zinazoweza kusaidia jamii kupunguza matumizi ya nishati zinazochafua mazingira.

Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Peter Kanuti Magari, akizungumza Agosti 12,2026 katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti hujuma na kulinda miundombinu ya umeme.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Peter Kanuti Magari, akizungumza Agosti 12,2026 katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti hujuma na kulinda miundombinu ya umeme.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mhandisi Peter Kanuti Magari, akizungumza Agosti 12,2026 katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti hujuma na kulinda miundombinu ya umeme.
Afisa Usalama Mkuu Msaidizi wa Uzuiaji TANESCO, Shami Yusuph Dunia, akizungumza katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti hujuma na kulinda miundombinu ya umeme.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Robert Msemo, akizungumza katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi Kahama
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Emma Nyaki, akizungumza katika kikao kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi Kahama.
Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Frank Njavike, akizungumza katika kikao cha TANESCO na Jeshi la Polisi kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme.

Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Katavi, Abeid Hamad Abeid, akizungumza katika kikao cha TANESCO na Jeshi la Polisi kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme.

Post a Comment

0 Comments