
Klabu ya Simba , imewatangazia mashabiki wake walionunua tiketi kuelekea mchezo wao wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Constantine watatumia tiketi hizo kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Masry ya Misri.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, hatua inayokuja kufuatia adhabu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) kwa klabu hiyo ya kucheza mechi moja bila mashabiki pamoja na faini ya Dola elfu 40,000.
CAF ilifanya uamuzi huo kufuatia vurugu zilizojitokeza katika mchezo wa CAFCC wa Simba Sc dhidi ya CS Sfaxien ya Algeria uliofanyika Disemba 15, 2024 katika dimba la Benjamin Mkapa.
“Wale wote ambao walinunua tiketi dhidi ya Constantine watatumia tiketi zao kwenye mchezo dhidi ya Al Masry.”—amesem Ahmed Ally
0 Comments