WAZIRI KABUDI AWAITA MEZANI YANGA, SIMBA, TFF NA BODI YA LIGI


Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amepanga kukutana na viongozi wa Shirikisho la mpira wa miguu TFF, Bodi la Ligi Kuu, Yanga na klabu ya Simba ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa ligi kuu bara baina ya Yanga na Simba

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi JumatatuMachi 24, 2025 kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam Alhamis na maofisa kutoka TFF, Bodi ya Ligi, Yanga pamoja na Simba wamejulishwa kuhudhuria

Wakati jitihada za kumaliza mgogoro huo mezani zikiendelea, tayari yanga imelipeleka suala hilo katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi ya michezo (CAS) baada ya kutoridhishwa na hatua iliyochukuliwa na bodi ya ligi kuahirisha mchezo dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa Machi 8, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa

Bodi ya ligi iliahirisha mchezo huo baada ya klabu ya Simba kutangaza kuwa haitacheza wakidai kuzuiwa kufanya maandalizi ya mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo huo

Kupitia matamko mbalimbali, wanachama wa Yanga wameweka msimamo na wamewaagiza viongozi wao kutokuwa tayari kurejeshwa tena uwanjani kucheza mchezo huo wakitaka hatua kali zichukuliwe kwa mujibu wa kanuni

Post a Comment

0 Comments