ABOUD AFUNGA KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM RUVUMA
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimehitimisha kampeni zake za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kata ya Ruvuma, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.
Hafla ya kufunga kampeni hizo imefanyika leo Novemba 26,2024 ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho, wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mohamed Aboud.
Katika hotuba yake, Aboud amewataka wakazi wa mkoa huo kuchagua viongozi wazuri watakaoweza kutatua changamoto na kero za wananchi, akisisitiza kuwa viongozi bora ni wale wanaotokana na CCM.
Aidha, Aboud amekubali mapendekezo ya Mbunge wa Viti Maalumu, Mariamu Nyoka, na Jackline Ngonyani (Msongozi), akisema yuko tayari kushirikiana nao kutatua changamoto mbalimbali, hasa za wanawake wa mkoa wa Ruvuma.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27,2024
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: