YANGA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA AZAM IKIWA NYUMBANI

Klabu ya Yanga leo imelazimishwa sare ya mabao 2 -2 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu NBC uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Feisal Salum 'Fei Toto' leo anastahili tuzo ya nyota wa mchezo kwa upande wa yanga akiwasaidia wananchi kuondoka na alama moja muhimu
Daniel Amoah aliitanguliza Azam FC kwenye dakika ya 24 baada ya mpira wa kichwa kumpita Diarra
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma ya goli 1-0 ambapo mkufunzi wa Yanga Nasreddine Nabi, alifanya mabadiliko wakati wa mapumziko kwa kuwaingiza Feisal Salum na Djuma Shaban katika nafasi ya Dickson Job na Denis Nkane
Mabadiliko hayo yaliisaidia Yanga kurejea mchezoni kwenye kipindi Feisali akiisawazishia Yanga goli dakika 56 ya kupitia shuti la nje ya 18
Changamoto ya krosi bado inaendelea kuitesa Yanga kwani mpira wa kona uliopigwa na Azam FC kwenye dakika ya 64 uliwasaidia kufunga bao la pili kupitia kwa Ndoye
Hata hivo Yanga ilirejea tena mchezoni baada ya kupata mkwaju wa penati Bernard Morisson akiangushwa kwenye eneo la hatari penati ambayo haikuwa bahati kwani Djuma Shaban alikosa
Dakika ya 76 wakati wananchi wakiwa katika hali ya kupoteza matumaini, Fei Toto akaachia shuti jingine nje ya 18 lililomshinda golikipa wa Azam Ahmad na kujaa nyavuni goli lililoleta usawa wa bao 2- 2 hadi dk 90 zilipokamilika.
Mchezo wa leo ulikuwa mchezo mgumu sana wenye upinzani mkali ambapo pengine matokeo hayo yanaakisi ugumu wa mpambano huo
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: