YANGA YAFUNGUKA UCHUNGU SUALA LA KISINDA, HATMA MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA

Kaimu mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga Simon Patrick amesema walikamilisha usajili wa Tuisila Kisinda kabla ya dirisha la usajili kufungwa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) iliwasaidia kupata ITC ya mchezaji huyo ndani ya muda
Patrick amebainisha kuwa baada ya kukamilisha usajili wa Kisinda waliiandikia barua kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuomba kumuondoa Lazarus Kambole katika orodha Y wachezaji waliosajiliwa na Yanga kwa ajili ya michuano ya ndani na nafasi yake kuchukuliwa na Kisinda
Yanga ilichukua uamuzi huo baada ya taarifa za kitabibu kubaini kuwa Kambole amepata majeraha ambayo yanaweza kumuweka nje kwa muda mrefu
Patrick amesema Kamati ya sheria na Hadhi ya wachezaji inayo mamlaka ya kufuta leseni ya muda iliyotolewa kwa Kambole ili kumpatia leseni Kisinda hivyo wanasubiri maamuzi ya Kamati hiyo ambayo inatarajiwa kukutana leo
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: