YANGA KUANZA KUSAKA UBINGWA WA 29 LEO
Wananchi wako mkoani Arusha ambapo jioni ya leo watashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo qa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2022/2023
Wakiwa ni mabingwa watetezi na mabingqa wa kihistoria wakishinda taji la Ligi kuu mara 29, leo wataianza kampeni ya kusaka ubingwa wa 29.
Kikosi cha kocha Nabi kilitua Arusha mapema jana na jioni wachezaji wakafanya mazoezi yao ya mwisho kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid.
Wananchi wataingia katika mchezo huo tayari wakiwa wameweka kibindoni taji la ngao ya Jamii wakiwachapa watani zao Simba 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi.
Mchezo wa leo utapigwa saa 10 kamili jioni
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: