PACHA WA PILI ALIYETENGANISHWA MUHIMBILI NAYE AFARIKI DUNIA







Pacha aliyesalia ‘Rehema’ kati ya mapacha wawili waliotenganishwa Julai Mosi 2022, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) amefariki dunia jana saa 5 asubuhi Agosti 11, wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma, Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, Rehema amefariki dunia siku 32 baadaye tangu kifo cha pacha wake ‘Neema’ kilichotokea Julai 10 mwaka huu.

Neema alifariki dunia baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa ICU na alizikwa Julai 14 katika makaburi ya Ulongoni B yaliyopo Gongo la Mboto.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.