MOLOKO KUWAAGA WACHEZAJI WENZAKE LEO
Klabu ya Singida big star imekubali kumlipa Jésus Ducapel Moloko mshahara na bonus kwa asilimia 40% na Yanga watamlipa mshahara Moloko asilimia 60% kwa msimu huu wote 2022-23.
Jésus Ducapel Moloko anatarajiwa kuwaaga wachezaji wenzie kambini leo Avic town mara baada ya mazoezi leo asubuhi na kuanza safari ya kwenda Singida kukamilisha taratibu za usajili wake ndani ya timu ya Singida big star.Kwa kandarasi ya miaka miwili 📃✍️.
Wakati Jésus Ducapel Moloko anatarajiwa kwenda mkoani Singida tayari Yanga nao wapo Katika hatua za mwisho kumalizana na Dario Federico da Silva jr maslahi binafsi(mshahara+bonus)na muda wowote kuanzia sasa atakuja jijini Dar es salaam kusaini mkataba 📃✍️.
Mkataba ambao Dario Federico da Silva jr anatarajiwa kusaini ndani ya Yanga ni wa muda wa miaka miwili.
🚨Dili zote mbili hizi za mabadilishano ya wachezaji zinaweza kutamatika kabla ya ijumaa kwa timu zote yaani Singida big star kumtangaza Jésus Ducapel Moloko na Yanga kumtangaza Dario Federico da Silva jr.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: