DIAMOND PLATNUMZ ATAJA KIWANGO CHA FEDHA AMBACHO ZUCHU ATATAKIWA KULIPA AKITAKA KUJIONDOA WCB
Baada ya Jana Agosti 15, 2022 Mbunge na Mlezi wa WCB kutangaza kupitia ukurasa wake wa instagram kwamba lebo ya Diamond inatarajia kutambulisha wasanii wawili watakaosainiwa hivi karibuni ila akaongezea kwa kusema kwamba safari msanii atakuwa na mashahidi wawili kutoka COSOTA na BASATA.
Sasa miongoni yaliyoibuka katika post hiyo iliyowekwa instagram zilimiminika maoni ya wadau mbalimbali na miongoni mwa walioandika ni Diamond Platnumz ambae yeye alicomment na kuandika “Mnataka mkawanyonye watu wengine eeh?.
Baada ya comment hiyo ya Diamond ziliibuka comments nyingi za mashabiki ikiwemo ya shabiki aliyemuuliza Diamond kwamba Kama Zuchu nae akitaka kuondoka WCB anatakiwa kulipa kiasi gani cha pesa? Diamond Platnumz alijibu kuwa "Huyo si chini ya 10 bilioni si unaona manamba huko you tube" alijibu Diamond
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: